- Hatua ya hakimu kumfunga jela maisha mtu wa daraja la chini zaidi aliyenaswa akisafirisha bangi huku matajiri wahalifu na wafisadi wakiachilia imezua tumbo joto nchini
- Wakenya wengi wanahisi kuwa idara hiyo ya mahakama inayoongozwa na Jaji Mkuu David Maraga inawapendelea wafisadi wakuu waliowaacha vijana bila kazi na katika hali ya mahangaiko
Hatua ya jaji mmoja katika kaunti ya mombasa ya kumfunga jela maisha kwa kupatikana akiwa amesafirisha bangi yenye thamani ya KSh 23, 250 imewaghadhabisha Wakenya.
Habari Nyingine: Mwanamke apigwa na butwaa baada ya kushikwa mkono na Rais Uhuru bila kutarajia (video)
Hukumu hiyo ilijiri saa chache tu baada ya mahakama kuwapa John Gakuo na Kirui, wote ambao walikuwa wafanyakazi wakuu serikalini, kifungo cha miaka mitatu tu gerezani kwa kosa la ubadhirifu wa KSh 283 milioni.

Habari Nyingine: Pasta awashangaza wengi akiwaamuru waumini kuvua chupi kanisani (video)
Kulingana na wengi wa Wakenya, idara ya mahakama inaonekana kuwa na sheria mbili na hukumu mbili zinazotofautiana; moja ya matajiri, na nyingine ya maskini.
Kulingana na hakimu mkuu Mombasa aliyetoa hukumu hiyo, Edgar Kagoni, mshukiwa huyo, Emmanuel Chacha alikuwa awaathiri vibaya vijana wa Mombasa kwa bangi yake, na hivyo hukumu ya kifungo cha maisha gerezani kilimstahili.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Wengi walishangaa ni kwa nini hukumu kama hizo hazingetumika kwa wanasiasa matajiri na wafanyabiashara wakuu nchini ambao uhusika kwa mambo sawia na hayo au hata zaidi.
Habari Nyingine: Kutana na kijana aliyemaliza chuo kikuu bila ‘kugusa’ msichana hata mmoja
Read ENGLISH VERSION
Una taarifa motomoto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke , kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko News
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibIFygZRmrpqjlaPGonnWmqOapJGirm631KGsrK1dncKswcyuZJ2tnp56u62MppihmZuWuqJ5w6GgnaFdrq5uw8Ccn6ibmKS5pnrHraSl